IQNA

Waislamu Marekani kuwakaribisha wasiokuwa Waislamu sikukuu ya Idi

15:49 - August 29, 2011
Habari ID: 2178858
Waislamu wa Marekani wameamua kuwakaribisha wasiokuwa Waislamu katika sikukuu ya Idul Fitr iliyopewa jina la Siku ya Milango Wazi ya Misikiti na Vituo vya Kiislamu.
Msemaji wa jumuiya ya ICNA ya Waislamu wa kaskazini mwa America Naeem Bing amesema kuwa katika siku hiyo itakayosadifiana na sikuu ya idi wataalikwa wasiokuwa Waislamu katika misikiti na vituo vya Kiislamu na kushuhudia kwa karibu mafundisho na sura halisi ya Uislamu katika siku hizi za kukaribia kumbukumbu ya Septemba 11.
Amesema kuwa moja ya njia muhimu za kuzuia tuhuma na hujuma zinazofanywa dhidi ya Waislamu ni kuanzisha uhusiano na wasiokuwa Waislamu na kuwashirikisha katika masuala na shughuli za Kiislamu. 851818

captcha