IQNA

Harakati za mapinduzi kuongezeka Saudia Arabia

15:07 - August 30, 2011
Habari ID: 2179143
Wananchi wa Saudi Arabia na hasa tabaka la vijana, wanafuatilia kwa karibu matatizo yanayowakabili ya kijamii na kiuchumi yakiwemo ya uhuru, umasikini na ubaguzi na jambo hilo linaweza kongeza harakati za mapinduzi nchini humo.
Raia na vijana wa Saudia wanafuatilia kwa karibu matatizo hayo kupitia mitandao ya kijamii ambapo wanajadili masuala nyeti ya kisiasa yanayoikabili nchi yao ukiwemo ukandamizaji unaofanywa dhidi yao na ukoo wa kifalme wa nchi hiyo.
Masuala kama vile ya ukosefu wa ajira, uhuru, elimu ya kutosha, uhaba wa huduma za afya na ukandamizaji wa uhuru wa kujieleza yanaoonekana wazi katika mijadala ya vijana hao kwenye mitandao hiyo ya kijamii.
Wanasiasa wanasema katika mitandao hiyo kwamba Saudi Arabia ni mojawapo ya nchi mbaya zaidi zinazokandamiza uhuru wa kijieleza na demokrasia duniani. 851934
captcha