IQNA

Ayatullah Qabalan avitaka vyama vya kisiasa vya Lebanon kufanya mazungumzo

11:58 - September 03, 2011
Habari ID: 2180336
Ayatullah Abdul Amir Qabalan, Naibu Mkuu wa Baraza Kuu la Mashia wa Lebanon amevitaka vyama vya kisiasa vya nchi hiyo kuimarisha umoja miongoni mwao na kufanya mazungumzo kwa ajili ya kukabiliana na changamoto na vilevile kutatua matatizo ya nchi hiyo.
Amewataka Walebanon pia kuimarisha umoja kati yao na kuisadia serikali katika uendeshaji wa nchi hiyo. Amesema vyama vya kisiasa havipasi kulichochea jeshi liingilie masuala ya kisiasa kwa sababu jukumu lake kuu ni kulinda maslahi ya taifa zima la Lebanon na kwamba wananchi wote wanatakiwa kulisaidia katika kukabiliana na vitisho vya kigeni vinavyohatarisha usalama wa nchi hiyo.
Amesisitiza kwamba jeshi, wananchi na mapambano ni nguzo tatu muhimu za nchi hiyo ambazo hazipasi kutenganishwa.
Ayatullah Qabalan ameongeza kuwa mawaziri wa serikali ya Leanon wanapasa kuweka pembeni tofauti zao na kujihusisha na mambo ya ujenzi wa taifa. 853419
captcha