IQNA

Wamagharibi wana wasiwasi kuhusu uundwaji wa serikali ya Kiislamu Libya

12:56 - September 04, 2011
Habari ID: 2181022
Katibu Mkuu wa Harakati ya Kiislamu ya Uokovu wa Libya amesema kuwa Wamagharibi wana wasiwasi mkubwa kuhusu suala la kuundwa serikali ya Kiislamu nchini humo na kusisitiza kuwa Walibya wanataka kuundwa serikali itakayosimama juu ya misingi ya sheria za Kiislamu.
Ibrahim Abdul Aziz Sahad amesema kuwa Walibya wanataka kuundwa serikali ya kidemokrasia, inayoheshimu utawala wa sheria na sheria za Kiislamu.
Amesisitiza kuwa serikali yoyote itakayotawala Libya na kudai kuwa inaheshimu haki na uhuru wa wananchi inapaswa kutilia maanani kwamba Walibya ni Waislamu.
Katibu MKuu wa Harakati ya Uokovu wa Libya amesema kuwa wasiwasi wa baadhi ya nchi za Magharibi juu ya kuwepo wanamgambo wa Kiislamu au kwamba wanaharakati wa Kiislamu wanadhibiti hali ya Libya hauna maana yoyote. 854038

captcha