Sheikh Hassan Saffar amelaani mashambulizi ya kigaidi yaliyotokea mwishoni mwa mwezi wa Ramadhani na katika siku ya Idul Fitri na kusababisha mauaji ya mamia ya Waislamu wasiokuwa na hatia.
Sheikh Saffar ambaye ni khatibu wa Swala ya Ijumaa ya Qatif nchini Saudi Araba amelaani vitendo vya kigaidi vilivyofanyika ndani ya misikiti na maeneo ya umma kama masoko huko Iraq, Pakistan, Nigeria, Afghanistan na Algeria ambayo yamesababisha mauaji ya Waislamu zaidi ya 240 na kusema kuwa sababu ya mashambulizi hayo ya kigaidi ni migogoro ya kisiasa, kiutamaduni na kijamii iliyopo katika jamii za Kiislamu.
Amesema vitendo hivyo vya kigaidi vinapingana na Uislamu na mafundisho ya dini hiyo.
Amesema wale wanaotoa fatua za kuhalalisha mauaji ya Waislamu na kutambua mauaji hayo kuwa ni halali nawashiriki katika kumwaga damu za watu wasiokuwa na hatia.
Maulamaa wa Kiwahabi wa Saudia Arabia wamekuwa wakitoa fatuwa za kuhalalisha mauaji ya Waislamu wa Kishia katika nchi mbalimbali hususan Iraq na Pakistan. 854183