IQNA

Dakta al Shahabi:

Hatima ya Mubarak na Gaddafi inawangojea watawala wa Bahrain

14:33 - September 06, 2011
Habari ID: 2182498
Katibu Mkuu wa Harakati ya Wapigania Uhuru wa Bahrain amesema kuwa utawala wa kizazi cha Aal Khalifa nchini humo utaporomoka kama zilivyoondolewa madarakani tawala za Hosni Mubarak huko Misri na Muammar Gaddafi huko Libya.
Said al Shahabi ameyasema hayo akizungumzia uwezekano wa kutolewa hukumu ya kifungo cha miaka 25 jela huko Bahrain dhidi ya Sheikh Muhammad Ali Mahfoudh ambaye ni Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Amal al Islami ya Bahrain. Amesema kuwa hatua ya utawala wa Aal Khalifa ya kumfunga jela Sheikh Muhammad Ali ni katika kudumisha ukandamizaji na dhulma za utawala huo.
Dakta al Shahabi amesema utawala wa Bahrain umevuka mipaka yote ya kibinadamu, kisiasa na kimaadili na haukubakisha ovu lolote.
Amesema utawala wa Bahrain umo katika hali ya kutoweka na kwamba wanamapambano na mashujaa wa Bahrain watapata ushindi kama alivyoahidi Mwenyezi Mungu SW.
Said al Shahabi pia ameashiria njama inayofanywa na utawala wa Bahrain ya kuwapa uraia wageni kwa ajili ya kubadili muundo wa jamii ya nchi hiyo na akasema kuwa ni vigumu kupata takwimu kamili za wageni wanaopewa uraia nchini Bahrain. Hata hivyo amesisitiza kuwa kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa miaka miwili iliyopita na pia matamshi ya baadhi ya maafisa wa serikali, idadi ya wageni waliopewa uraia kwa shabaha ya kuvuruga muundo wa jamii ya Bahrain ilikuwa watu laki moja na nusu. 855589
captcha