IQNA

Kuwapa watoto majina mazuri, kuwafunza Qur’ani ni jukumu la wazazi

22:04 - September 06, 2011
Habari ID: 2182643
Imam Ali AS amesema: ‘Kina baba wana jukumu la kuwapa watoto majina yanayofaa, kuwalea vizuri na kuwafunza Qur’ani.’
Ulezi unamaanisha kuwa kutoa mafunzo ya kieleimu na kitabia ili watoto waweza kutambua vipawa vyao na kuwa na mwelekeo bora kwa msingi wa Uislamu. Kwa mujibu wa Uislamu, elimu huanzia katika uundwaji wa familia yaani wakati wa kumchagua mume au mke utakayeishi naye katika kipindi chote cha maisha.
Elimu kwa watoto imetiliwa mkaza sana na Uislamu hata kabla ya kuzaliwa. Mtume SAW anasema: ‘Aliyebarikiwa ni yule ambaye saada yake imeainishwa akiwa tumboni na aliye na mashaka ni ambaye masaibu yake yalianza kabla hajazaliwa’.
Kuhusu majukumu ya wazazi kwa watoto Imam Sajjad AS anasema: ‘Unapaswa kujua watoto wako, wawe wabaya au wazuri katika dunia hii na unawajibika kwao kuhusu tabia zao na kuwaelekeza katika njia ya Mwenyezi Mungu na kuwasaidia wamuombe kwani utapata thawabu ukifanya hivyo na utaadhibiwa ukifanya kinyume. Wafunze kwa njia ambayo wataonyesha ushawishi wako na tekeleza majukumu yako kwao na waelekeza wamtii Mwenyezi Mungu’. Vilevile Imam Sadiq AS anasema: "Acha watoto wacheze hadi wafike umri wa miaka saba, wafunze kwa miaka saba na shauriana nao kama wasaidizi wako katika miaka saba inayofuata katika maisha yao’.
854399
captcha