Makala hii inalenga kuangazia maudhui za mazingira katika Qur’ani na Sunna na vilevile sababu zinazochangia kuchafuka mazingira. Aidha makala hiyo inapendekeza mikakati ya kimaadili, kiuchumi, kifiqhi na kiafya ambayo inaweza kutumika kulinda mazingira.
Mwandishi wa makala anaashiria aya ya 30 ya sura ya 21 ya Qur’ani Tukufu isemayo: "Na tukajaalia kwa maji kila kilicho hai". Anasema maji ndio elementi muhimu zaidi ya maisha ya viumbe vyote wakiwemo wanadamu, wanyama na mimea kwa hivyo kuna haja ya kuwepo mikakati ya kulinda vyanzo vya maji.
Aidha anajadili hatua ya baadhi ya wanadamu kutojali suala la kulinda mazingira. Anasema kupuuzwa mazingira kunaweza kuwa tishio kwa uhai wa viumbe.
854248