IQNA

Kesi ya Firauni wa Misri yaendelea mjini Cairo

22:56 - September 07, 2011
Habari ID: 2183400
Kesi ya Firauni wa zama wa Misri dikteta Hosni Mubarak, wanawe wawili, waziri wa mambo ya ndani wa zamani na maafisa kadhaa wa ngazi za juu wa masuala ya usalama imeendelea leo mjini Cairo chini ya ulinzi mkali wa polisi na askari usalama.
Kikao cha leo cha kesi ya Firauni wa Misri kilisikiliza ushahidi uliotolewa na maafisa usalama wa zamani kuhusu amri ya kuwapa silaha polisi na amri ya kuwafyatulia risasi raia wakati wa maandamano ya wananchi yalimuondoa madarakani Hosni Mubarak.
Vikao vya kesi ya rais wa zamani wa Misri vilianza juzi kwa kusikiliza ushahidi kuhusu mauaji ya raia wakati wa mapinduzi ya wananchi wa Misri mapema mwaka huu.
Dikteta Mubarak na jamaa zake wanatuhumiwa kwa kuamuru mauaji dhidi ya raia, kutumia vibaya madaraka yao na kupora mali ya umma. Firauni wa Misri anakabiliwa na hukumu ya kifo iwapo atapatikana na hatia. 856690




captcha