Akizungumzia masuala muhimu ya Lebanon, Sheikh Naim Qasim amesema kwamba chama cha Mustakbal na mrengo wa Machi 14 wana changamoto muhimu na tata za kiuchumi, kisiasa na kijamii zinazowasubiri. Amesema, Walebanon wanajivunia jeshi, taifa na Hizbullah na kwamba ukweli huo haupaswi kupuuzwa na mtu yoyote.
Naibu Katibu Mkuu wa Hizbullah amesema kuwa wafuasi wa chama hicho wanaheshimu na kutekeleza vilivyo sheria na katiba ya nchi hiyo, katika mazingira yoyote yale.
Sheih naim Qasim amesema kuwa Hizbullah haitaki kuona Lebanon ikidhoofika kwa maslahi ya utawala haramu wa Israel na kwamba juhudi zozote zile za kuvuruga utulivu na umani hazioani na katiba ya nchi hiyo. 856790