IQNA

Misimamo ya kindumakuwili ya Qaradhawi kuhusu mapinduzi ya eneo

12:57 - September 13, 2011
Habari ID: 2186122
Sheikh Yusuf Qaradhawi Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Maulamaa Waislamu amechukua misimamo ya kindumakuwili kuhusu matukio yanayojiri katika ulimwengu wa Kiarabu.
Kwa upande mmoja anaunga mkono wanaozusha ghasia nchini Syria na kuikosoa vikali serikali ya nchi hiyo na kwa upande wa pili anayataja mapinduzi ya wananchi wa Bahrain kuwa ni fitina.
Kwa mujibu wa televisheni ya Al Alam, Qaradhawi hivi karibuni katika mahojiano aliyofanyiwa alifumbia macho mauaji yanayofanya na vikosi vya utawala wa Aal Khalifa wa Bahrain unaopata himaya ya utawala wa Aal Saud.
Qaradhawi amedai kuwa serikali ya Syria inawaua watu wasio na ulinzi. Aidha amewalaumu maulamaa wakubwa wa Syria kwa kuunga mkono serikali ya Rais Bashar al Assad.
859561
captcha