Kwa mujibu wa duru za habari za Israel Danny Navon pamoja na wafanyakazi wake wameondoka nchini Jordan. Wanaharakati nchini Jordan waliandaa maandamano ya watu milioni moja jana ambayo yamepangwa kuanza saa kumi na mbili na nusu jioni kwa majira ya nchi hiyo karibu na ubalozi wa utawala wa kizayuni.
Hayo yanajiri kufuatia maandamano makubwa dhidi ya Israel yaliyofanyika siku ya Ijumaa iliyopita katika mji mkuu wa Misri Cairo ambapo waandamanaji waliuvamia ubalozi wa utawala huo haramu na kubomoa sehemu za ukuta wa zege uliozunguka ubalozi huo.
Kwa mujibu wa gazeti la Jerusalem Post maandamano ya Jordan yalifanyika kwa sha'ar isemayo" Ubalozi wa Kizayuni hautakiwi katika ardhi ya Jordan".
Hapo jana wananchi wa Jordan walikusanyika mbele ya ubalozi wa Marekani mjini Amman na kuchoma moto bendera za Israel na Marekani na kutaka nchi yao ivunje uhusiano wake na pande hizo mbili za Tel Aviv na Washington. 861603