Wanachama 15 wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wamekubali kwa kauli moja kutumwa kikosi cha UN nchini Libya ili kusaidia taifa hilo kurejea katika hali ya kawaida baada ya kupinduliwa utawala wa Muammar Gaddafi.
Vilevile Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeliondolea vikwazo vya kifedha Shirika la Mafuta la Libya na Benki Kuu ya nchi hiyo. Imeamuliwa kuwa fedha zote za Libya zilizofungiwa ziachiliwe huru na kutumiwa kwa faida ya wananchi wa Libya.
Kwa mujibu wa azimio lililopitishwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, wawakilishi wa Baraza la Mpito la Libya wanaweza kushiriki katika mkutano wa mwaka wa Baraza Kuu kama wawakilishi rasmi wa serikali ya Tripoli. 862049