Televisheni ya al Alam imeripoti kuwa, askari usalama wa Bahrain waliwashambulia waanamanaji hao na kujeruhi mmoja miongoni mwao.
Raia kadhaa pia walipatwa na hali ya kubanwa na pumzi kutokana na gesi iliyokuwa ikitumiwa na askari usalama wa utawala wa kifalme wa Aal Khalifa.
Maandamano hayo ya wananchi wa Bahrain yamefanyika kupinga mauaji ya Jafar Hassan Yusuf aliyefariki dunia kutokana na mateso aliyopewa na polisi ya nchi hiyo.
Raia huyo alifariki dunia Jumamosi iliyopita. 863429