Kikao hicho kitafanyika kwa ushirikiano wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu OIC, Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la nchi za Kiislamu ISESCO, na Wizara ya Elimu ya Juu ya Saudia.
Lengo la kufanyika kikao hicho ni kujadili hati itakayochunguza sera kuu za utendaji na miongozo kwa ajili ya kunyanyua viwango vya elimu katika vyuo vikuu vya nchi za Kiislamu.
Mazungumzo ya duara pia yatafanyika pambizoni mwa kikao hicho chini ya anwani ya 'kuimarisha ushirikiano wa nchi za Kiislamu katika sekta ya elimu ya juu na uboreshwaji viwango.'
Udharura wa kifanyika kikao hicho ulihimizwa mwaka uliopita katika kikao cha tano cha Mawaziri wa Elimu ya Juu wa nchi wanachama wa OIC huko Malaysia. Vikao vya kabla ya hapo vilifanyika Riyadh mwaka 2002, Tripoli Libya 2003, Kuwait 2006, Baku Azerbaijan 2008 na Kuala Lumpur mwaka uliopita wa 2010. 870358