Maro Amadou amesema, maafisa wa Baraza la Taifa la Mpito la Libya ambalo limetambuliwa rasmi na serikali ya Niamey wanaweza kwenda Niger na kumsaili Saadi Gaddafi.
Ameongeza kuwa suala hilo halina maana kwamba serikali ya Niger itamkabidhi Saadi Gaddafi kwa viongozi wa Libya.
Saadi Gaddafi alikimbilia nchini Niger baada ya kusambaratika serikali ya baba yake Muammar Gaddafi ambaye hajulikani aliko. 871275