IQNA

Duru ya nane ya kikao cha wakuu wa ukusanyaji kodi na masuala ya zaka yafanyika

14:46 - October 03, 2011
Habari ID: 2198142
Duru ya nane ya kikao cha Muungano wa Wakuu wa Kodi na Masuala ya Zaka wa Nchi za Kiislamu ilifanyika jana Jumapili huko Riyadh, mji mkuu wa Saudi Arabia.
Kwa mujibu wa tovuti ya spa, kikao cha utangulizi cha kikao hicho cha jana kilifanyika siku ya Jumamosi ambapo washiriki walijadili masuala mbalimbali yaliyopangwa kupewa umuhimu katika kikao cha jana.
Kikao cha Riyadh kilitilia mkazo umuhimu wa kuimarishwa mawasiliano na kuunganishwa sheria za kiraia na kidini kuhusiana na suala la zaka. Washiriki walisisitiza umuhimu wa kushirikiana maafisa husika wa masuala ya ukusanyaji kodi na zaka ili kuimarisha masuala hayo katika nchi za Kiislamu. Wamesema udharura wa jambo hilo unatokana na ukweli kwamba kodi na zaka zina nafasi muhimu katika ustawi na maendeleo ya nchi.
Nchi 28 wanachama wa muungano uliotajwa zimetaka kupewa uanachama katika Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu OIC. Vikao vingine kama hicho cha Saudia vilifanyika katika miaka iliyopita katika nchi za Malaysia, Iran, Pakistan, Kuwait, Indonesia na Sudan. 872132
captcha