IQNA

Hotuba za Sayyid Nasrullah zinaitia kiwewe Tel Aviv

14:50 - October 05, 2011
Habari ID: 2199582
Mtaalamu wa saikolojia wa Israel amekiri kwamba Kiongozi wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon Sayyid Hassan Nasrullah alianzisha vita vikali ya kinafsi dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel kwa hotuba zake kali na uwezo wake mkubwa wa kuhutubia wakati wa vita vya pili vya Lebanon, suala ambalo lilikuwa na taathia kubwa katika ushindi wa Hizbullah dhidi ya Israel.
Tesvy Gell ameandika kuwa hotuba kali zilizotolewa na Sayyid Nasrullah wakati wa vita vya pili vya Israel dhidi ya Lebanon mwaka 2006 zilianzisha vita vya kisaikolojia dhidi ya utawala huo ghasibu na kutoa mchango mkubwa katika ushindi wa wanamapambano wa Hizbullah dhidi ya Israel.
Mtaalamu huyo wa masuala ya kinafsi wa Israel ameongeza kuwa Katibu Mkuu wa Hizbullah angali anaongoza vita vya kisaikolojia dhidi ya Israel na ana sifa zote anazopaswa kuwa nazo kiongozi mwenye mafanikio.
Tesvy Gell ambaye aliwahi kufanya kazi kama mtaalamu wa saikolojia katika jeshi la Israel amesema kuwa Sayyid Hassan Nasrullah ni hodari mno katika vita vya kinafsi dhidi ya Israel na hotuba zake zinawakinaisha watu wengi hasa ndani ya Israel.
Amesema idadi ya hotuba za televisheni za kiongozi wa Hizbullah ni ndogo na kwa njia hiyo huwafanya walimwengu wasubiri kwa hamu kusikia maneno na hotuba yake ijayo, na hiyo ndiyo siri ya mafanikio ya shakhsia huyo. 873956

captcha