Msikiti huo utakaojengwa kwenye uwanja wa hekari 7.5 utakuwa na minara minne yenye urefu wa mita 65 na ukuba la mita 47. Gharama ya ujenzi wa msikiti huo imekisiwa kuwa ya dola milioni 100 ambapo milioni 70 zitatolewa na Qatar na zilizobaki kutolewa na Tajikistan yenyewe.
Sherehe ya uzinduzi wa ujenzi wa msikiti huo ilifanyika Alkhamisi kiliyopita na kuhudhuriwa na Rais Imamali Rahman wa nchi hiyo.
Baadhi ya wachambuzi wa mambo wanasema kuwa rais huyo ameamua kujenga msikiti huo ili kutuliza hasira za Waislamu wa nchi hiyo ambao wanahisi kukandamizwa na serikali kuhusiana na masuala ya kidini.
Hivi karibuni Rais Rahman alipiga marufuku watoto kuhudhuria misikitini na wanawake kuingia kwenye shule, vyuo vikuu na idara za serikali wakiwa wamevalia hijabu, jambo lililowakasirisha sana Waislamu. Asilimia 98 ya Watajiki ni Waislamu. 875287