IQNA

Mufti wa Misri aitwa 'munafiki' katika Swala ya Ijumaa

16:02 - October 08, 2011
Habari ID: 2201002
Ali Jumua, Mufti wa Misri alituhumiwa na baadhi ya waumini walioshiriki kwenye Swala ya Ijumaa hapo jana kuwa munafiki alipokuwa akitoa hotuba za swala hiyo.
Kwa mujibu wa gazeti la al-Quds al-Arabi linalochapishwa mjini London Uingereza, baadhi ya waumuni waliohudhuria swala hilo iliyoswaliwa katika mji wa Port Said walipaza sauti zao wakimtuhumu mufti huyo kuwa ni munafiki na mmoja wa mabaki na vibaraka wa utawala wa dikteta Hosni Mubarak aliyeng'olewa madarakani hivi karibuni.
Ali al-Juheimi aliyeanzisha nara za kumtuhumu mufti huyo alijaribu kumshambulia mufti lakini akazuiliwa na waumini wenzake na kuondolewa nje ya msikiti.
Wanazuoni wengine wa Misri ambao walikuwa wakishirikiana kwa karibu na utawala wa Mubarak, wamekuwa wakishambuliwa na wananchi katika siku za hivi karibuni na kutuhumiwa kuwa wanajaribu kufanya njama za kuteka nyara mapinduzi yao. 875385
captcha