Afisa mmoja wa polisi ya Uingereza ambaye aliongoza operesheni ya kutiwa nguvuni watu hao amesema kuwa, operesheni hiyo ilikuwa kama mashindano ya mbio za nyika.
Christopher Greny amesema kuwa timu kubwa ya askari iliundwa kwa ajili ya kuwakamata watu walioshiriki katika machafuko ya mwezi Agosti mjini London na kuzuia yasienee katika miji mingine.
Ameongeza kuwa picha za video zimetumika kuwatia nguvuni watu walioshiriki katika machafuko hayo.
Awali Scotland Yard ilitangaza kuwa watu 2952 walitiwa nguvuni katika machafuko hayo. 875720