Zaidi ya viongozi wanawake 150 Waislamu kutoka nchi 45 duniani watakutana katika mkutano huo utakaofanyika chini ya anwani ya 'Viongozi Wanawake Waislamu katika Mstari wa Mbele wa Mageuzi'. Mkutano huo utasimamiwa na Jumuiya ya Ubunifu wa Kiislamu ya Wanawake (WISE) na Taasisi ya Marekani ya Maendeleo ya Waislamu (ASMA).
Mkurugenzi Mtendaji wa jumuiya ya ASMA Daisy Khan amesema kuwa lengo la mkutano huo ni kuhalalisha harakati ya kimataifa na maendeleo ya wanawake wa Kiislamu
Mkutano huo utajadili nafasi muhimu ya wanawake katika nyanja mbalimbali za kisiasa, masuala ya miji, biashara na masuala ya kiroho na kimaanawi.
Mkutano huo pia utahudhuriwa na mshauri maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Nafis Siddiq na jaji wa kwanza mwanamke wa Kipalestina Khulud al Faqiih. 875647