Habari zinasema kuwa magari ya kijeshi ya Saudia yalianza kuuzingira mji wa Qatif hiyo jana na kwamba sasa mji huo unazingirwa kikamilifu.
Uchunguzi umebaini kuwa magari hayo ya kijeshi yametoka katika kituo cha jeshi la Saudi Arabia cha Dhahran na kwamba idadi nyingine ya magari hayo iko njiani kuelekea Qatif.
Majeshi yaliyotumwa katika mji huo wenye idadi kubwa ya Mashia yanajumuisha askari polisi, askari wa kuzima ghasia na jeshi la gadi ya ufalme wa Saudia.
Maeneo yenye idadi kubwa ya wafuasi wa madhehebu ya Shia ya mashariki mwa Saudi Arabia kwa siku kadhaa sasa yanashuhudia maandamano makubwa yanaokabiliwa na mashambulizi ya askari usalama. Maandamano hayo yalianza baada ya imam wa Swala ya Ijumaa katika Msikiti Mtakatifu wa Madina Sheikh Ali al Hudhaifi kuwavunjia heshima wafuasi wa madhehebu ya Shia akiwaita kuwa ni makafiri.
Wataalamu wa masuala ya kisiasa wa Saudia wanatabiri kwamba upinzani na malalamiko ya Mashia nchini humo huenda yakashadidi zaidi iwapo shekhe huyo wa Kiwahabi hataomba radhi.
Mashia wa Saudi Arabia ambao wamekuwa chini ya dhulma na ukandamizaji kwa miaka mingi, wanadai haki zao za kimsini ikiwa ni pamoja na uhuru wa kueleza itikadi zao na uhuru wa kuabudu. 877159