IQNA

Wapinzani wa utawala wa Bahrain watakiwa kuunda serikali

21:43 - October 11, 2011
Habari ID: 2203279
Ayatullah Sheikh Muhammad Sanad ambaye ni marjaa na mwanazuoni mkubwa wa Kiislamu wa Bahrain anayeishi katika mji mtakatifu wa Najaf huko Iraq amewataka wapinzani wa utawala wa kifalme wa Bahrain waunde serikali ya wananchi kwa ajili kufikia malengo yao.
Taarifa iliyotolewa na mwanazuoni huyo mkubwa wa Kiislamu imesema kuwa wapinzani wa serikali ya kifalme ya Bahrain wanahitaji kuwa na ushirikiano, umoja na mshikamano kwa ajili ya kuweza kukabiliana na utawala wa kizazi cha Aal Khalifa.
Ayatullah Sanad amesisitiza juu ya kuwa na umoja na udharura wa kuanzisha serikali ya wananchi huko Bahrain.
Amesema kuwa makundi ya upinzani yanapaswa kutambua kwamba jamii ya kimataifa na nchi za Mashariki ya Kati zinafanya mazungumzo na wapinzani wa utawala wa Kifalme wa Bahrain ambao ndio wawakilishi halisi wa wananchi.
Ameongeza kuwa suala hili linazisha haja ya kuundwa serikali ya wananchi ndani ya nje ya nchi ambazo zitaendesha harakati za mapambano katika medani za kimataifa. 878037

captcha