Rasimu ya sheria mpya ya uchaguzi ya Lebanon ilichunguzwa hapo jana Jumanne kwa kuhudhuriwa na Sayyid Hassan Nasrullah, Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapabano ya Kiislamu Hizbullah pamoja na Waziri wa Mambo ya Ndani wa nchi hiyo.
Kikao hicho ambacho pia kilihudhuriwa na Haj Wafiq Swafa, Mkuu wa Idara ya Uratibu ya Hizbullah, baada ya kuchunguza rasimu hiyo kilijadili pia matukio na masuala ya kisiasa na kiusalama ya Lebanon na eneo zina la Mashariki ya Kati.
Katibu Mkuu wa Hizbullah pia siku hiyohiyo ya Jumanne alionana na kuzungumza na Omar Karami, Waziri Mkuu wa zamanai wa Lebanon na vilevile Faisal Karami, Waziri wa Michezo na Vijana wa nchi hiyo ambapo walijadili na kuzungumzia masuala mahimu ya kisiasa ya Lebanon na ya kieneo. 878328