Msemaji wa Kamisheni Kuu ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa amelitaka pia jeshi la Misri kuwalinda raia wote wa Misri wakiwemo wafuasi wa dini za waliowachache.
Rupert Colville amesema kuwa kamisheni hiyo inawataka viongozi wa Misri wachukue msimamo huru na usiopendelea upande wowote katika uchunguzi wa matukio ya Maspero.
Ripoti nyingine zinasema kuwa Baraza la Makanisa ya Mashariki ya Kati limetoa taarifa likilaani machafuko na ghasia za Misri na limewataka viongozi wa nchi hiyo kuchukua hatua kali za kurejesha amani na utulivu nchini himo.
Watu 24 waliuawa na mamia ya wengine kujeruhiwa katika ghasia za Jumapili iliyopita katika eneo la Maspero mjini Cairo zilizohusisha Wakristo wa Kikopti na askari usalama. 878370