Amesema hayo leo mwanzoni mwa safari yake ya kutembelea mkoa wa Kirmanshah wa magharibi mwa Iran ambako amepata mapokezi ya aina yake ya makumi ya maelfu ya wananchi wa mkoa huo.
Amesema, harakati ya kimapinduzi ya wananchi wakiwemo wa nchi za Tunisia, Misri na Libya ni majibu kwa siasa za miaka mingi za tawala za nchi za eneo hili za kuwa vibaraka wa Marekani na madola ya kibeberu.
Amesisitiza kwamba, leo hii mazingira ni mengine na hali katika eneo hili imebadilika kabisa.
Ayatullahil Udhma Khamenei amesema pia kwamba, ijapokuwa Marekani inafanya njama za kudhibiti hali hiyo lakini mataifa ya eneo hili yameshaamka na Marekani haiwezi kukabiliana na maamuzi ya wananchi wa mataifa hayo.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amebainisha pia taathira za ajabu za mwamko wa mataifa ya dunia na huku akitolea mfano silisila ya matukio yanayoendelea kushuhudiwa katika nchi za Ulaya na Marekani ameisema kuwa, matukio hayo ni mfano mwingine wa mabadiliko yanayoendelea kushuhudiwa hivi sasa duniani kiasi kwamba wananchi wa Marekani nao wameamua kusimama na kufanya maandamano ya kupambana na mfumo ulioshindwa wa kibepari katika nchi za Magharibi.
Ayatullahil Udhma Khamenei ameongeza kuwa, maandamano makubwa ya wananchi wa Marekani yaliyoenea katika zaidi ya miji elfu moja nchini humo ni ushahidi wa wazi wa kushindwa mabavu bandia ya madola ya Magharibi mbele ya maamuzi ya wananchi. 878859