IQNA

Harakati ya kuteka Wall Street ina taathira kubwa

14:47 - October 15, 2011
Habari ID: 2205147
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Washington nchini Marekani amechunguza na kujadili mwenendo wa harakati ya kuteka nyara Wall Street na taathira zake katika uchaguzi ujao wa rais na kusisitiza kuwa hapana shaka kuwa harakati hii itakuwa na taathira katika kubadili hali ya sasa nchini Marekani.
Kituo cha habari cha Klewtv kimeripoti kuwa T.V Read mtaalamu wa harakati za kijamii na mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Washington amesema kuwa malalamiko ya wananchi wa Marekani yatakuwa na taathira kubwa kwani kama inavyoshuhudiwa sasa mazungumzo na maamuzi yanayohusiana na masuala ya uchumi hapa nchini yamebadilika, na hii ni moja ya malengo muhimu ya harakati ya kuteka nyara Wall Street.
Mhadhiri huyo wa Marekani ameongeza kuwa katika harakati ya sasa kunashuhudiwa mshikamano mkubwa kati ya vijana na jumuiya za wafanyakazi kiasi kwamba nishati kubwa ya vijana na itibari na uungaji mkono wa jumuiya za wafanyakazi vitabadilisha mlingano wa kiuchumi nchini Marekani.
880017
captcha