Huku maandamano ya wananchi wa Yemen dhidi ya utawala wa kidikteta wa Rais Ali Abdullah Saleh yakishadidi, maafisa usalama wa nchi hiyo wameua waandamanaji 12 na kujeruhi makumi ya wengine katika mji mkuu wa nchi hiyo, Sana'a.
Mapambano makali yameripotiwa kutokea katika wilaya ya Hassaba kati ya vikosi vya watu wa makabila na vikosi vinavyomuunga mkono dikteta Saleh.
Ali Abdullah Saleh alirejea nchini Yemen Septemba 23 akitokea Saudia, alikokwenda kutibiwa kutokana na majeraha aliyopata kufuatia shambulizi la bomu dhidi ya ikulu mwezi Juni.
Mamia ya Wayemen wameuawa na maelfu ya wengine kujeruhiwa tangu yalipoanza maandamano dhidi ya serikali mapema mwezi Januari mwaka huu. 880172