Taarifa iliyotolewa na Ban Ki Moon imeeleza kwamba Ban Ki-moon anakaribisha makubaliano yaliyofikiwa na kusema kwamba ana matumaini kuwa mzingiro wa Gaza utamalizika hivi karibuni.
Katibu Mkuu wa UN amesema kuwa kubadilishana mateka kati ya Hamas na Israel ni hatua muhimu katika njia ya kurejesha amani Mashariki ya Kati.
Amesema anatajia kwamba Israel itachukua hatua mpya za kukomesha mzingiro wa Gaza na kulijenga upya eneo hilo.
Amezipongeza pia nchi za Misri na Ujerumani ambazo zimechangia katika kufikiwa makubaliano hayo ya kubadilishana mateka. 883320