Ayatullahil Udhma Ali Khamenei alisema hayo Jumatano katika siku ya nane ya kutembelea mkoa wa Kermanshah wa magharibi mwa Iran mbele ya umati mkubwa wa wakazi wa Kangavar.
Ameongeza kuwa, mashetani wanajua vyema kwamba mataifa yaliyoamka ya eneo la Mashariki ya Kati na kaskazini mwa Afrika yamelikodolea macho ya matumaini taifa la Iran na ni kwa sababu hiyo ndio maana mashetani hao wanafanya njama kubwa kwa kutumia mbinu na suhula zao zote ili kujaribu kuzuia Iran na Wairani wasiwe kigezo kwa harakati adhimu ya mwamko wa Kiislamu iliyojitokeza hivi sasa katika eneo hili.
Ayatullah Khamene pia amesema, lengo la njama hizo za maadui ni kuipaka matope Iran kupitia kukuza kupindukia udhaifu unaotekezea hapa na pale nchini na kufifilizisha au kunyamazia kabisa maendeleo makubwa inayoendelea kupata Iran kila leo.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran ameongeza kuwa, kinachomuunguza na kumteketeza adui ni kuona kuwa, kutokana na Mapinduzi ya Kiislamu, Iran imetoka katika sifa yake ya kuwa kituo kikuu cha kutii amri za adui na sasa imekuwa ni nchi na taifa lililosimama imara kupambana na mabeberu na linaendelea kukabiliana vilivyo na ubeberu na siasa za kupenda makubwa za adui kwa heshima na uhuru kamili, bila ya kuogopa chochote.883158