Msikiti huo ambao utakuwa mkubwa zaidi nchini Algeria umepangwa kujengwa katika mji mkuu wa nchi hiyo Algiers. Msikiti huo unatazamiwa kugharimu euro bilioni moja. Utajengwa kwenye uwanja ulio na ukubwa wa hekari 20 na minara yake itakuwa na urefu wa mita 300.
Msikiti huo utakuwa na sehemu ya kuswalia ambayo itakuwa na uwezo wa kubeba watu 40,000 na ukumbi mwingine ulio na uwezo wa kubeba watu 80,000.
Msikiti huo utakuwa wa tatu kwa ukubwa baada ya Masjidul Haram mjini Makka na Masjidu Nabi (saw) mjini Madina.
Msikiti huo mpya utakaopewa jina la al-Jazeera utakuwa na maktaba ya gorofa 15, taasisi ya utafiti wa Kiislamu na pia jumba la maonyesho ya sanaa na historia ya Kiislamu. Minara ya msikiti huo itakuwa na urefu wa mita 100 zaidi kuliko minara ya Msikiti wa Mfalme Hassan II nchini Morocco, ulioko katika mji wa Daru Beidhaa. 883169