IQNA

Semina ya Ghadir kufanyika Uingereza

22:22 - October 22, 2011
Habari ID: 2209576
Semina ya Ghadir imepangwa kufanyika tarehe 13 Novemba katika Kituo cha Kiislamu nchini Uingereza.
Semina hiyo itajadili maana ya uongozi wa Kiislamu katika mitazamo mbalimbali, Ghadir katika mtazamo wa Ahlusunna, Ghadir katika mtazamo wa kihistoria wa Mashia na Ghadir na maana ya uongozi wa Kiislamu.
Mwishoni mwa semina hiyo washiriki wataulizwa swali kwamba je, kama wangeishi katika zama za Bwana Mtume (saw) wangetekeleza maneno yaliyosemwa na mtukufu huyo siku ya Ghadir Khum au la? 884537

captcha