Televisheni hiyo ilifunguliwa mashtaka baada ya kurusha hewani filamu ya Persepolis inayovunjia heshima matukufu ya Kiislamu na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Mashtaka hayo yaliwasilishwa mahakamani na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Tunisia, mawakili 144 na raia kadhaa wa nchi hiyo.
Hata hivyo Mwendesha Mashtaka Mkuu wa serikali ya Tunisia amekataa ombi la chama kimoja cha siasa nchini humo ambacho kilikuwa kimetaka kufungwa matangazo ya Televisheni ya Nasma hadi baada ya uchaguzi wa leo wa Baraza la Waasisi.
Baada ya televisheni hiyo kurusha hewani filamu ya katuni inayoonyesha picha iliyodaiwa kuwa ni ya Mwenyezi Mungu, Waislamu wa Tunisia walifanya maandamano makubwa wakipinga kitendo hicho kinachovunjia heshima matukufu ya Kiislamu. 885175