IQNA

Ghanushi aonya kuhusu udanganyifu katika uchaguzi wa Tunisia

15:03 - October 23, 2011
Habari ID: 2210212
Katibu Mkuu wa Harakati ya al Nahdha al Islami ya Tunisia ametahadharisha kuhusu uwezekano wa kufanyika udanganyifu katika uchaguzi wa leo wa Baraza la Waasisi.
Rashid al Ghanushi ametishia kwamba iwapo kutafanyika udanganyifu wa aina yoyote katika uchaguzi wa leo wananchi wa Tunisia watamiminika tena mitaani.
Wananchi wa Tunisia leo wameelekea kwenye masanduku ya kupigia kura katika uchaguzi wa kwanza huru tangu baada ya kung'olewa madarakani utawala wa kidikteta wa Zainul Abidin bin Ali. Katika uchaguzi wa leo Watunisia wanawachagua wawakilishi 218 wa Baraza la Waasisi. 885310
captcha