Wanazuoni hao pia wameharamisha kushiriki kwa vibaraka hao katika uchaguzi ujao wa bunge ambao umepangwa kufanyika nchini tarehe 27 Novemba.
Akifafanua suala hilo, Sheikh Omar Sutuhi, Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Uhubiri wa Kiislamu ya al-Azhar amesema kuwa haijuzu kwa raia yoyote wa Misri kumuozesha binti yake kwa mwanachama wa Chama cha Taifa cha Misri ambacho ni chama tawala cha zamani cha nchi hiyo.
Sheikh huyo amesema kuwa kila Mmisri aliye na ghera na kujivunia dini na taifa lake hapasi kumpigia kura mwanachama wa chama kilichotajwa cha kisiasa na hasa ikitiliwa maanani kwamba chama hicho kimefanya ubadhirifu mkubwa katika mali ya umma na kudhoofisha Misri katika upeo wa kimataifa.
Sheikh Omar Sutuhi ameongeza kuwa kila mtu atakayewapigia kura wanachama wa chama hicho kilichopigwa marufuku atahesabiwa kuwa msaliti wa nchi yake.
Vilevile amewataka Wamisri wote kuwa waangalifu kuhusiana na suala hilo hasa katika kipindi hiki cha kukaribia uchaguzi nchini. 885553