IQNA

Sheikh Salman:

Waislamu wa Kishia wanaendelea kushambuliwa katika mimbari

16:45 - October 26, 2011
Habari ID: 2212460
Imam na khatibu wa msikiti wa Aal al Rasul (saw) katika mkoa wenye Waislamu wengi wa madhehebu ya Shia wa Ihsaa huko mashariki mwa Saudi Arabia amesema kuwa inasikitisha kuona kwamba mwenendo wa kuwavunjia heshima Waislamu wa Kishia katika mimbari bado unaendela.
Sheikh Hashim Salman amesema kuwa kuchochea ugomvi kati ya Waislamu ni jambo la kusikitisha mno na linalozusha mivutano kati ya wafuasi wa madhehebu mbalimbali.
Amesema kuwa ochochezi huo wa kimadhehebu unafanyika zaidi dhidi ya Waislamu wa madhehebu ya Shia.
Sheikh Salman amekosoa pia hotuba iliyotolewa na hatibu wa Msikiti wa al Ahmadi nchini Kuwait akishambulia Mashia na kuvunjia heshima matukufu yao.
Amesema kuwa Mashia ni zaidi ya thuluthi moja ya Waislamu wote duniani na ni jambo lisilokubalika kuvunjia heshima idadi kubwa kama hiyo ya Waislamu kwa kuzitaja itikadi zao kuwa ni uzushi na upotofu. Amesisitiza kuwa jambo kama hilo litakuwa na taathira mbaya.
Sheikh Hashim Salman amewataka Waislamu wa Kishia wanaokwenda Makka kwa ajili ya ibada ya Hija kulinda amani na utulivu na kutojali matamshi na hotuba zinazotaka kuzusha hitilafu na mifarakano kati ya Waislamu. 887756

captcha