IQNA

Maonyesho ya 'Uislamu Nchini Uingereza' yaendelea

12:51 - October 27, 2011
Habari ID: 2212714
Maonyesho ya 'Uislamu Nchini Uingereza' yanaendelea katika Kituo cha Mfungamano wa Kimataifa RISC mjini Berkshire.
Maonyesho hayo ambayo yamepangwa kuendelea hadi tarehe 30 Novemba yanaonyesha mambo mbalimbali yanayohusiana na nchi za Kiislamu katika nyanja tofauti za kielimu, lugha, usanifu majengo, mavazi na mambo mengine mengi.
Maonyesho hayo pia yanachunguza athari ya Uislamu kwa Uingereza.
Waandaaji wa maonyesho hayo wanasema kuwa yana umuhimu mkubwa kwa kutilia maanani kwamba yanawarejesha wageni wanaoyatembelea katika zama za kale ambapo Waislamu walikuwa na nguvu kubwa duniani kutokea kaskazini mwa Afrika hadi India.
Wamesema katika zama hizo, Waislamu walikuwa na vyuo vikuu na vituo muhimu vya kielimu na kupiga hatua kubwa za maendeleo ya kielimu katika hali ambayo nchi za Magharibi zilikuwa zingali nyuma katika nyanja za elimu na teknolojia. 887711
captcha