IQNA

Ayatullah Jannati:

Walimwengu wameanzisha mapambano dhidi ya mfumo wa kibepari

18:01 - October 29, 2011
Habari ID: 2213842
Khatibu wa sala ya Ijumaa iliyosaliwa leo mjini Tehran amewataka watawala wa White House nchini Marekani wajifunze kutoka katika historia na kuacha udanganyifu wa kisiasa. Ayatullah Jannati amesisitiza kuwa, walimwengu wameanza kupambana na mfumo wa kibepari.
Huku akiashiria mwamko wa Kiislamu katika nchi za Mashariki ya Kati na kaskazini mwa Afrika, Ayatullah Ahmad Jannati amesema kuwa, watawala wa Marekani wanapaswa kujifunza kutokana na historia kwani haiwezekani kukabiliana na watu kwa mabavu.
Ayatullah Jannati aidha amesema Marekani baada ya miaka 10 ya kuikalia kwa mabavu Iraq na kuua raia wengi wasio na hatia wa nchi hiyo na pia kuharibu miundo mbinu ya nchi hiyo, hivi sasa imelazimika ikubali kuondoka nchini humo.
Khatibu wa sala ya Ijumaa ya leo ya hapa mjini Tehran pia amesema kuwa, harakati ya 'Wall Street' nchini Marekani na katika nchi nyinginezo duniani ni muqawama wa wananchi wa dunia dhidi ya mfumo wa kibepari, ambapo tabaka kubwa la watu yaani asilimia 99 wamesimama kupambana na tabaka la kibepari ambalo ni asilimia moja tu lakini linadhibiti kila kitu.
888542
captcha