Televisheni ya al Alam imenukuu watu walioshuhudia wakisema kuwa shambulizi la kwanza la ndege za kivita za utawala ghasibu wa Israel limelenga ofisi ya Batalioni ya Qassam katika eneo la Zaitun, huko mashariki mwa Gaza.
Shambulizi hilo limesababisha hasaha za kimaada lakini halikusababisha mauaji.
Shambulizi la pili la ndege za kijeshi za Israel lililenga kituo cha mafunzo cha Batalioni ya Qassam kusini magharibi mwa eneo la Khan Yunis na kusababisha hasara za kimaada.
Jana ndege za kivita za Wazayuni wa Israel pia zilishambulia eneo la Gaza na kuua shahidi Wapaletina 9 wanachama wa Batalioni ya Quds.
Batalioni ya Quds ambayo ni tawi la kijeshi la harakati ya Jihad Islami na makundi mengine ya mapambano ya ukombozi ya Palestina yalijibu mashambulizi hayo kwa kurusha maroketi kadhaa dhidi ya maeneo ya Wazayuni. 889615