Kamanda Othman Al Ghanimi amesema Khamis al Kartani na wasaidizi wake 9 wametiwa nguvuni katika operesheni kubwa iliyofanyika katika mji huo mtakatifu.
Ameongeza kuwa katika operesheni hiyo askari usalama wa Karbala wamekamata pia magari mawili yaliyokuwa yametegwa mabomu kwa ajili ya kulipuliwa, karakana ya kutengeneza guruneti, kilogramu 700 za mada za milipuko na maroketi 32.
Kamanda wa jeshi la polisi ya Karbala amesema mtandao wa kigaidi wa al Al Qaida ulikuwa ukijitayarisha kwa ajili ya kutekeleza mashambulizi ya mabomu katika mji huo mtakatifu.
Amesema kuwa Khamisi al Kartani alihusika na mashambulizi yaliyotokea siku za hivi karibuni dhidi ya Waislamu anaokwenda kuzuru Haram ya mjukuu wa Mtume Muhammad (saw) Imam Hussein (as). 889702