Al Maliki amesema kuwa mkoa huo umekuwa maficho ya amani kwa mabaki ya utawala ulioondolewa madarakani wa Kibaath na magaidi.
Waziri Mkuu wa Iran amesema kuwa mfumo wa utawala wa federali ni suala la kisheria lakini kutangazwa kadhia hiyo sambamba na kutoa tuhuma dhidi ya serikali na kuzungumzia hitilafu za kimadhehebu na chama cha Baath ni jambo linalotia shaka kubwa.
Nouri al Maliki ameutaja mkoa wa Salahuddin kuwa ni sawa na moto unaotokota chini ya majivu na kuongeza kuwa wafuasi wa dikteta wa zamani wa Iraq wanataka kuufanya mkoa huo kuwa makimbilio ya amani kwa makundi ya kigaidi. 889932