IQNA

Askari Waislamu wa Ufaransa waliouawa katika Vita vya Kwanza vya Dunia kukumbukwa

10:32 - October 31, 2011
Habari ID: 2214876
Shughuli ya kuwakumbuka askari Waislamu wa Ufaransa waliouawa katika Vita vya Kwanza vya Dunia itafanyika tarehe 10 Novemba katika mji wa Lyon.
Kituo cha habari cha Mosquee-lyon kimeripoti kuwa shughuli hiyo itasimamiwa na Msikiti wa Lyon na itahudhuriwa na viongozi wa serikali akiwemo Meya wa Lyon, maulamaa, maimamu wa Swala za jamaa na raia Waislamu na wasiokuwa Waislamu.
Hadhirina watazuru makaburi ya askari Waislamu wa Ufaransa waliouawa shahidi katika Vita vya Kwanza vya Dunia na kuwaombea dua.
Viongozi wa serikali ya Ufaransa pia watahutubia hadhara hiyo wakizungumzia mchango wa askari Waislamu katika kulinda mipaka ya nchi hiyo wakati wa Vita vya Kwanza vya Dunia.
Zaidi ya askari laki moja Waislamu waliuawa shahidi katika Vita vya Kwanza na vya Pili vya Dunia wakilinda mipaka ya Ufaransa. 890350


captcha