Tamasha hilo ambalo lilianza Ijumaa iliyopita litaendelea hadi kesho Alkhamisi. Tamasha hilo ambalo limemsifu Muhammad Bu Azizi, Mtunisia ambaye alianzisha mapinduzi yanayoendelea hivi sasa katika nchi kadhaa za Kiarabu kwa kujichoma moto kulalamikia dhulma ya watawala wa Kiarabu, lilipata fursa ya kunufaika na maneno ya familia yake ambayo ilikuwa imesafiri nchini Ufaransa kupokea zawadi ya Sakharov ya Umoja wa Ulaya.
Mashindano ya kidini na kiutamaduni, maonyesho ya picha za maeneo ya Kiislamu na pia mapinduzi ya Tunisia, Libya na Misri ni sehemu ya ratiba za tamasha hilo.
Kuarifishwa Waislamu wapya wa Ufaransa, hotuba za wanazuoni wa kidini kuhusiana na fadhila za Idul Adh'ha, hotuba za wasomi na wanafikra kuhusiana na hali ya Waislamu nchini Ufaransa na nafasi ya matamasha pamoja na maonyesho mbalimbali ya Kiislamu katika kuimarisha umoja miongoni mwa Waislamu wanaoishi barani Ulaya ni miongoni mwa mambo yanayofuatiliwa kwa karibu na waandaji wa tamasha hilo. 891922