IQNA

Ayatullahil Udhma Khamenei:

Marekani ndiye gaidi mkubwa duniani

20:56 - November 02, 2011
Habari ID: 2216719
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, leo Jumatano asubuhi ameonana na maelfu ya wanafunzi na wanachuo hapa mjini Tehran katika muda huu wa kukaribia tarehe 13 Aban (yaani Novemba 4) ambayo nchini Iran inahesabiwa kuwa ni siku ya mwanafunzi na siku ya taifa ya kupambana na ubeberu duniani.
Ayatullahil Udhma Khamenei amekumbushia njama mbali mbali zilizofanywa na mabeberu wa dunia wakiongozwa na Marekani na Uzayuni wa kimataifa dhidi ya taifa la Iran na kusisitiza kuwa, wasiwasi walio nao maadui hivi sasa ni kuona mataifa mengine yanazifanya fikra makini na madhubuti za kisiasa za mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuwa kigezo bora kwao.
Ameongeza kwamba, baada ya kutumbukia kwenye matatizo makubwa yanayoongezeka kila leo hususan baada ya kuanza harakati kubwa ya wananchi iliyopewa jina la "Wall Street" huko nchini Marekani kwa ajili ya kupinga mfumo wa kibepari, viongozi wa White House wamezuka na tamthilia ya kuchekesha dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran wakieneza madai ya uongo ya kuituhumu Iran kuhusika na kitendo kisicha na maana cha ugaidi, bila mantiki yoyote.
Amesema, kila mtu mwenye akili timamu na mweledi wa mambo duniani, wameipinga vikali tamthilia hiyo ya kuchekesha iliyozushwa na serikali ya Marekani dhidi ya Iran.
Ameongeza kuwa, moja ya malengo ya tamthilia hiyo mpya ya Marekani ni kujaribu kuficha athari za harakati ya kupinga ubepari ya "Wall Street" dhidi ya Marekani na vile vile kuishinikiza zaidi Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Amesema: Wamarekani wamezusha njama hizo ili kuipaka matope nembo kubwa ya mapambano duniani yaani Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kupitia kuituhumu kuhusika na ugaidi katika hali ambayo leo hii gaidi mkubwa duniani ni Marekani yenyewe.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kwamba: Iran ina hati mia moja ambazo hazina dosari yoyote ili kuthibitisha nafasi ya Marekani katika kuongoza mauaji ya kigaidi nchini Iran na katika eneo la Mashariki ya Kati ambapo kama hati hizo mia moja tutazitangaza duniani, basi bila ya shaka yoyote heshima ya Marekani na ya watu wanaodai kupigania haki za binaadamu na kupambana na ugaidi duniani itaondoka kabisa mbele ya walimwengu.
captcha