IQNA

Ayatullah Issa:

Wanaozusha fitina baina ya Shia na Suni wanapuuza ubinadamu

21:12 - November 05, 2011
Habari ID: 2217955
Khatibu wa swala ya Ijuma ya Bahrain amesema kuwa watu wanaochochea fitina za kimadhehebu kati ya Waislamu wa madhehebu za Shia na Suni wanapuuza dini, ubinadamu na matukufu yote.
Ayatullah Issa Qasim aliyasema hayo jana katika hotuba za Swala ya Ijumaa mjini Manama na akawataka Wabahrain kutotumbukia katika moto wa fitina za kimadhehebu.
Amesema kuwa watu wanaochochea moto wa fitina za kimadhehebu wanataka kuwasha moto wa pande zote kwa ajili ya kuutumia vibaya na kudhibiti hali ya mambo kwa maslahi yao. Amesisitiza kuwa maisha na mali ya wananchi haina thamani yote kwa watu wa aina hii.
Khatibu wa Swala ya Ijumaa ya Manama ameuambia utawala wa kifalme wa Bahrain kwamba ni jinai kubwa ya kisiasa kuzusha fitina za kimadhehebu kati ya wananchi.
Vilevile amewahimiza Waislamu wa madhehebu za Shia na Suni kujiepusha na fitina hizo.
893248


captcha