Mkurugenzi Mkuu wa taasisi hiyo Yasin Hamoud ameiandikia barua UNESCO akiitaka kunda turathi za Kiislamu za Quds Tukufu mbele ya mashambulizi yanayofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel na kuzuia kuharibiwa turathi hizo kwa kutayarisha orodha na nyaraka zinazohusiana na maeneo ya Kiislamu na ya kale ya mji wa Quds.
Amesema UNESCO inapaswa kuchukua hatua haraka iwezekanavyo na kuzuia uharibifu unaofanywa na Israel dhidi ya turathi za Kiislamu za Quds Tukufu.
Yasin Hamoud amesema kuwa uanchama wa Palestina katika shirika la UNESCO ni hatua muhimu katika kutetea haki za wananchi wa Palestina na kwamba anatarajia kwamba shirika hilo litawasilisha sauti ya Wapalestina kwa walimwengu. 894016