IQNA

Mahitaji ya Tafsiri za Qur’ani kwa Kiswidi yaongezeka baada ya tukio la kuvunjia heshima nakala ya Qur’ani

15:50 - December 28, 2025
Habari ID: 3481729
IQNA – Baada ya tukio la kuvunjia heshima nakala ya Qur’ani Tukufu mbele ya Msikiti Mkuu wa Stockholm, mahitaji ya kununua tarjuma au tafsiri za Qur’ani kwa lugha ya Kiswidi yameongezeka kwa kiwango kikubwa.

Kwa mujibu wa ripoti ya Alkompis, baada ya tukio la kuchoma nakala Qur’ani mbele ya Msikiti Mkuu wa Stockholm, maombi ya kununua tafsiri ya Qur’ani Tukufu kwa Kiswidi yaliongezeka sana, na huenda hili likawa moja ya athari chanya zilizotokana na tukio hili la kusikitisha nchini Uswidi au Sweden.

Kwa miaka mingi kumekuwepo na tafsiri kadhaa za Qur’ani nchini Sweden, na watu wengi wamejitahidi kuwasilisha maana na dhana za Qur’ani Tukufu kwa Waislamu wa nchi hiyo ya Ulaya.

Kwa sasa, zipo tafsiri au tarjuma 8 tofauti za Qur’ani kwa Kiswidi, tafsiri ya kwanza ikifanywa katika karne ya 18 na ya mwisho katika miaka ya hivi karibuni.

Baada ya kuanzishwa kwa Scandinavian Education Foundation mnamo Desemba 3, 2022, hatua maalum zilichukuliwa kuelekea kutafsiri Qur’ani Tukufu.

Kila tarjuma ya Qur’ani kwa Kiswidi ina tofauti zake na nyingine, na jambo la kushangaza ni kwamba zaidi ya nusu ya tafsiri zilizopo zilitolewa na Waswidi wasio Waislamu na wafuasi wa dini nyingine, ikiwemo Uyahudi na Ukristo. Walifanya hivyo kwa sababu walikuwa na hamu ya kujifunza kuhusu Qur’ani na pia walihisi jukumu kwa jamii yao, hivyo wakatafsiri Qur’ani Tukufu kwa Kiswidi na kuichapisha.

3495872

Habari zinazohusiana
Kishikizo: qurani tukufu uswidi
captcha