IQNA

Safdari miongoni mwa Maqari wa Iran waliofuzu Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani Qatar

21:27 - January 05, 2026
Habari ID: 3481768
IQNA – Reza Safdari, qari mashuhuri kutoka mkoa wa Sistan na Baluchestan, kusini mashariki mwa Iran, amejiunga na kundi la wanaofuzu kuingia fainali za mashindano ya kimataifa ya Qur’ani yanayofanyika nchini Qatar.

Safdari tayari ameondoka kuelekea Doha, mji mkuu wa Qatar, kwa ajili ya kushiriki katika mashindano hayo yenye hadhi kubwa katika ulimwengu wa Qur’ani.

Hapo kabla, Safdari aliwahi kushika nafasi ya kwanza katika mashindano ya wanafunzi wa Qur’ani, na pia amehudhuria kambi maalumu ya kuchagua wawakilishi wa Iran kwa mashindano ya kimataifa ya Qur’ani kwa wanafunzi wa ulimwengu wa Kiislamu.

Aidha, amewahi kusoma Qur’ani mbele ya Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu na katika vituo mbalimbali vya Shirika la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran (IRIB).

21:27 - 2026/01/05

Waliofuzu hatua ya fainali ya mashindano ya kimataifa ya Qur’ani nchini Qatar wametokana na zaidi ya washiriki 3,000 waliojitokeza katika hatua za awali.

Washiriki hao wanatoka katika mataifa mbalimbali, yakiwemo Misri, Morocco, Indonesia, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Malaysia, Afghanistan, Qatar, Saudi Arabia, Umoja wa Falme za Kiarabu, Pakistan, Libya, Nigeria, Ufaransa, Urusi, Tajikistan na Jamhuri ya Azerbaijan.

Kwa mujibu wa Safdari, makari wengine wawili kutoka Iran wanaoshiriki mashindano hayo ni Mehdi Gholamnejad na Seyed Mostafa Hosseini.

“Natumai tutakuwa wawakilishi wazuri wa nchi yetu tukufu ya Kiislamu, Iran, katika mashindano haya,” aliongeza.

3495958

captcha