Katika video hiyo, Sheikh Nuaina, ambaye ni Sheikh al-Qurra au Qari bingwa wa Misri, anaonekana akimfundisha mwanamke huyo kutamka Shahada kama hatua ya kuingia katika Uislamu. Watu wengi waliokuwepo msikitini walijibu tukio hilo kwa kutamka kwa sauti “Takbir” (Allahu Akbar, yaani Mungu ni Mkubwa).
Video hiyo ilipokelewa kwa pongezi nyingi kutoka kwa mashabiki na wafuasi wa ukurasa wa Sheikh Nuaina.
Aidha, Sheikh Nuaina alipokuwa mgeni katika kipindi cha televisheni Dawlat al-Tilāwah alitoa maelekezo muhimu kwa mshiriki Omar Ali, akisisitiza umuhimu wa kuhifadhi Qur’ani kwa mwendelezo.
Qari huyo wa Misri, ambaye pia ni daktari kwa taaluma, alisema kwamba haitoshi kuhifadhi Qur’ani bila kuikariri mara kwa mara, kwani kufanya hivyo huzuia udhaifu wa kuhifadhi na kusaidia kuepuka kusahau aya.

Alisisitiza umuhimu wa kutenga muda maalumu kila siku kwa ajili ya kusoma Qur’ani, akifafanua kuwa kusoma angalau sura tano kwa siku humsaidia mhifadhi kuimarisha uhifadhi wake na kuendeleza uhusiano wake na Kitabu cha Mwenyezi Mungu.
Sheikh Nuaina pia aliwashauri maqari au wasomaji wa Qur’ani kuanza kwa sauti ya chini na kutochosha mishipa ya sauti, ili waweze kuendelea kusoma bila kuchoka au kupata maumivu.
Qari huyo mashuhuri alisisitiza kuwa unyenyekevu, usomaji wa mara kwa mara, kurudia kwa uthabiti, pamoja na kuheshimu Kitabu cha Mwenyezi Mungu, ndizo sifa halisi za msomaji yeyote anayetaka kuinua kiwango chake na kupata usomaji unaokubalika mbele ya Mwenyezi Mungu.
3495957